21
Watakatifu Mtii
Kwa shauku
1. Watakatifu mtii
Mwamuzi mkuu.
Andaa njia ya Bwana;
Sasa yu karibu.
Andaeni meza kuu,
Wote waje kula.
Tazama Bwana Harusi
Aja kwa adhama.
2. Mwombeni Bwana kwa sala
Ili wanadamu
Waupokee ufalme
Na wote wasifu.
Funguo zimerejeshwa;
Injili sambaza,
Wekeni wazi ukweli
Umefunuliwa.
3. Utukufu wake Bwana
Wawaka Sayuni,
Maana ndiyo mnara;
Naye ni mlezi.
Watakatifu fuata
Nyayo za mababu.
Kwa nyoyo za shukurani
Tumuenzi Mungu.
Maandishi: Ed M. Rowe, 1878–1951. © 1948 IRI
Muziki: Robert P. Manookin, 1918–1997. © 1948 IRI