92
Ninainamisha Kichwa
Kwa sala
1. Ninainamisha kichwa
Na kukuwaza Mwokozi.
Sakramenti nachukua
Kuikumbuka ahadi.
2. Nakusihi nikumbushe
Ulinifia Golgotha,
Ili nikue milele
Niishi na wewe, Bwana.
3. Macho yangu nainua,
Kuangalia mbinguni,
Ili niweze kujua
Nifanyeje kustahili.
4. Niishivyo duniani,
Nipe Roho nikaweze
Kubadilika moyoni,
Na kukua kama wewe.
Maandishi: Zara Sabin, 1892–1980. © 1985 IRI
Muziki: Thomas L. Durham, kuz. 1950. © 1985 IRI