Muziki
Sote Ni Askari


143

Sote Ni Askari

Kwa shauku

1. Sote ni askari, dhambi tuzishinde;

Tufurahi! Tufurahi!

Taji la utukufu tutazamie;

Tutalishinda taratibu.

Hima vitani, kaza mwendo;

Ukweli daima ni ngao.

Ona bendera ivumavyo!

Kwa shangwe, shangwe twarudi kwetu.

[Chorus]

Sote ni askari dhambi tuzishinde;

Tufurahi! Tufurahi!

Taji la utukufu tutazamie;

Tutalishinda taratibu.

2. Sikia! Mbiu yalia kwa sauti;

Itikia! Itikia!

Tunasubiri askari; U tayari?

Msalabani kusanyika.

Aita Jemedari wetu;

Usichelewe, usihofu!

Pigania Mwokozi wetu;

Kwa shangwe, shangwe twarudi kwetu.

[Chorus]

Sote ni askari dhambi tuzishinde;

Tufurahi! Tufurahi!

Taji la utukufu tutazamie;

Tutalishinda taratibu.

3. Tunapigania falme ya mbinguni;

Tufurahi! Tufurahi!

Twaimba twendavyo; kheri tu askari,

Punde ushindi tutapata.

Hatari zaja – Je, tuhofu?

Kiongozi daima, Yesu.

Faraja, na Mlinzi wetu.

Kwa shangwe, shangwe twarudi kwetu.

[Chorus]

Sote ni askari dhambi tuzishinde;

Tufurahi! Tufurahi!

Taji la utukufu tutazamie;

Tutalishinda taratibu.

Maandishi: Hajulikani, The New Golden Chain, New York, 1866

Muziki: William B. Bradbury, 1816–1868

2 Timotheo 2:3; 4:7–8

Waefeso 6:10–18