51 Pokea Ibada Yetu Kwa unyenyekevu 1. Pokea ibada yetu Na Roho anong’one. Tujaze hisia Yesu, Na furaha ikue. Uwe wetu, uwe wetu, Hata mbio tushinde, Uwe wetu, uwe wetu, Hata mbio tushinde. 2. Tufanye uyatakayo. Mahitaji utupe, Pia tupe Roho wako Ili juu tufike. Utulinde, utulinde Hadi nasi tushinde. Utulinde, utulinde Hadi nasi tushinde. 3. Na siku ya ufufuo Dhambi utuepushe, Kwenye ufufuko wako Tufufuke na wewe. Tukusifu, tukusifu Hata milele yote. Tukusifu, tukusifu Hata milele yote. Maandishi: Richard Alldridge, 1815–1896 Muziki: Joseph J. Daynes, 1851–1920 Waebrania 12:1–2 Mafundisho na Maagano 59:23