23
Sayuni Nzuri Mbinguni
Kwa upole
1. Sayuni nzuri mbinguni;
Napenda mji mzuri;
Mizuri milango yake;
Hekalu – Mungu nuruye;
Aliyenipatanisha,
Milango aifungua.
[Chorus]
A! Sayuni, ni kuzuri;
Mji Sayuni;
Sayuni, kwake Mungu!
2. Kuzuri mbinguni kote;
Hata malaika wote;
Nzuri nazo tumbuizo;
Nzuri tarumbeta zao;
Nitaimba na umati,
Miguuni pa Mwokozi.
[Chorus]
A! Sayuni, ni kuzuri;
Mji Sayuni;
Sayuni, kwake Mungu!
3. Mazuri mataji yao,
Matawi watandazayo;
Wazuri wakombolewa,
Wote wanaoingia;
Nitaingia kwa hamu
Kwenye pumziko langu.
[Chorus]
A! Sayuni, ni kuzuri;
Mji Sayuni;
Sayuni, kwake Mungu!
Maandishi: George Gill, 1820–1880
Muziki: Joseph G. Fones, 1828–1906