24
Katika Siku ya Shangwe
Kwa furaha
1. Katika siku ya shangwe,
Bwana, twakutukuza;
Hapa ni patakatifu,
Utukufu twaimba.
[Chorus]
Haleluya, Haleluya,
Sauti tuzitoe,
Tuimbeni kwa furaha
Kwa Bwana na Mfalme!
2. Ifungue chemichemi;
Zimwagike baraka,
Kwa wakutumikiao
Kwenye hii dunia.
[Chorus]
Haleluya, Haleluya,
Sauti tuzitoe,
Tuimbeni kwa furaha
Kwa Bwana na Mfalme!
3. Tujenge ufalme wako,
Alisema nabii,
Kwamba wana wa ahadi
Ndipo watapoishi.
[Chorus]
Haleluya, Haleluya,
Sauti tuzitoe,
Tuimbeni kwa furaha
Kwa Bwana na Mfalme!
Maandishi na Muziki: Leroy J. Robertson, 1896–1971. © 1980 IRI