18
Tumpendao Mungu
Kwa furaha
1. Tumpendao Mungu,
Njooni kwa furaha.
Tumwimbie nyimbo tamu,
Tumwabudu pamoja.
2. Kuna wale wageni
Wasiojua neno.
Sisi ndio watumishi
Wakutangaza kwao.
3. Mungu ni Mtawala
Wa dunia na mbingu,
Kwa kauli hutuliza
Dhoruba na ghadhabu.
4. Huyu Mwenyezi Bwana,
Ndiye upendo wetu,
Nguvu zake atatuma
Kutupeleka juu.
Maandishi: Isaac Watts, 1674–1748
Muziki: Aaron Williams, 1731–1776