179
Tuliishi kwa Baba
Kwa urahisi
1. Kweli hapo kale tuliishi kwa Baba
Tukipendwa na watu tuliowajua.
Ndipo Mungu akaleta mpango wake
Wa wokovu na wa maisha ya milele.
2. Baba alitaka mwenye pendo la kweli
Wa kutukomboa ili kwake turudi.
Mwingine alitaka heshima tukufu.
Yesu alisema, “Utukufu kwa Mungu.”
3. Yesu akatumwa kuja kama Masiya;
Kwa jina lake Ibilisi akashindwa.
Anatupa matumaini ya kuishi
Mbinguni kwa Baba anakotusubiri.
Maandishi na Muziki: Janeen Jacobs Brady, kuz. 1934
© 1987 na Janeen Jacobs Brady. Wimbo huu ni kwa matumizi ya kawaida, ya kanisa yasiyo ya kibiashara au matumizi ya nyumbani.