97
Baba Yetu Twaamini
Kwa ujasiri
1. Baba yetu twaamini
Ahadi za kwako;
Tunapokea injili,
Wema wasemavyo.
2. Tunatubu zetu dhambi
Pia kwako twaja.
Agano tunakubali
Kuchagua mema.
3. Kubali maombi, Bwana,
Na utusamehe,
Tukawe viumbe wapya
Na dhambi tuache.
4. Sakramenti twapokea
Kwa jina la Kristo,
Ili tupate mwangaza
Kwenye maagano.
5. Kwenye maji twazamishwa
Kwa jina la Yesu,
Tufufuke na mwangaza
Wa Roho wa Mungu.
6. Utubatize kwa Roho,
Wana wako tuwe,
Tukawe pamoja nao
Wateule wote.
Kwa sakramenti, imba ubeti 1–4.
Kwa ibada ya ubatizo, usiimbe ubeti wa 4.
Maandishi: Parley P. Pratt, 1807–1857, yamebadilishwa.
Muziki: Jane Romney Crawford, 1883–1956