12
Mungu Mbariki
Kwa sala
1. Mungu mbariki
Mpendwa nabii,
Mpe afya.
Na utuongoze sote
Kwa maneno yake,
Ili tuchague
Yale mema.
2. Na wako ufalme,
Uenee pote
Ufikapo.
Ukweli wawaka,
Nasi twaungana,
Kwa kasi kufika
Kwenye lengo.
3. Tuwe na umoja,
Kama Baba, Mwana,
Kwa amani.
Kwa mioyo yote,
Tusimame sote,
Na milele tuwe
Majasiri.
Maandishi: Bernard Snow, 1822–1894
Muziki: Harry A. Dean, 1892–1987.© 1985 IRI