Muziki
Roho wa Mungu


2

Roho wa Mungu

Kwa kushangilia

1. Roho wa Mungu awaka kama moto!

Utukufu wa zama hizi waja;

Zarudi baraka za kale, maono,

Na malaika wazuru dunia.

[Chorus]

Tutaimba nao majeshi ya mbingu

Hosana, hosana Mungu na Kristo!

Utukufu wapewe walio juu

Sasa na milele yote, Amina!

2. Bwana atuongezea ufahamu,

Kama mwanzo, mwamuzi arejeshwa.

Waongezeka na uwezo wa Mungu;

Pazia linaanza kupasuka.

[Chorus]

Tutaimba nao majeshi ya mbingu

Hosana, hosana Mungu na Kristo!

Utukufu wapewe walio juu

Sasa na milele yote, Amina!

3. Kusanyiko la kiroho tutaita,

Na kueneza ufalme wa mbingu,

Kwa imani tutaanza kurithishwa

Baraka na utukufu wa Mungu.

[Chorus]

Tutaimba nao majeshi ya mbingu

Hosana, hosana Mungu na Kristo!

Utukufu wapewe walio juu

Sasa na milele yote, Amina!

4. Siku ya ajabu watakapolala

Kondoo na simba bila ghadhabu,

Efrahimu Sayuni kutunukiwa,

Kwa garimoto ashukapo Yesu!

[Chorus]

Tutaimba nao majeshi ya mbingu

Hosana, hosana Mungu na Kristo!

Utukufu wapewe walio juu

Sasa na milele yote, Amina!

Maandishi: William W. Phelps, 1792–1872. Yalijumuishwa katika kitabu cha kwanza cha nyimbo za Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho, 1835. Yaliimbwa wakati wa kuweka wakfu, Hekalu la Kirtland mwaka 1836.

Muziki: Hajulikani, mnamo 1844

Mafundisho na Maagano 109:79–80

Mafundisho na Maagano 110

Chapisha