35
Mungu wa Baba Zetu wa Kale
Kwa shauku
1. Mungu wa baba zetu wa kale,
Mkonowe watawala kote,
Twaimba nyimbo za shukurani
Mbele ya Kiti chako cha Enzi.
2. Upendowe ulituongoza;
Nchi hii huru umetupa.
Kuwa Mlinzi, Mlezi wetu,
Njia zako ziwe njia zetu.
3. Vitisho vya vita na taabu,
Mkono wako utunusuru.
Dini yako safi itujae.
Wema wako uturutubishe.
Maandishi: Daniel C. Roberts, 1841–1907
Muziki: George W. Warren, 1828–1902
Zaburi 33:12