129
Fanya Muda Mzuri
Kwa upole
1. Fanya muda mzuri
Na usikupite.
Wakati wa mchana
Kazi zifanyike.
Hatuwezi amuru
Utulie mwanga.
Au vivuli vingi
Ghafla kutoweka.
2. Muda unapepea;
Nyuma haurudi.
Unasogea mbele
Kwenye njia nzuri.
Tusipolifahamu,
Muda hupotea,
Maisha hayarudi,
Kama vile jana.
3. Baada ya baridi
Linakuja joto,
Na huzuni zikija
Furaha haipo.
Si yatupasa basi
Leo kujaribu,
Kufikia malengo
Kuacha uvivu?
4. Fanya muda mzuri;
Utumie sasa.
Kuitika upesi
Huleta baraka.
Hekima iongoze;
Uwe mwaminifu;
Mungu akubariki
Uwe mkarimu.
Maandishi na muziki: Robert B. Baird, 1855–1916