1. Njoo kwa Yesu, ulemewaye,
Usumbukaye nazo dhambi,
Akuongoze upumzike
Kwao wenye imani.
2. Njoo kwa Yesu, atakupata
Japo gizani, mpotevu.
Upendo wake utaongoza
Ufike kwenye nuru.
3. Njoo kwa Yesu, atasikia,
Ukimuomba pendo lake.
Je unajua na malaika
Wako karibu nawe?
4. Njoo kwa Yesu, kila taifa,
Katika ulimwengu huu.
Kwetu wote wa hii dunia,
Aita “Njoo kwangu.”