48 Karibu Na Ewe, Mungu Wangu! Kwa upole 1. Karibu na Ewe, Mungu wangu! Ingawa mateso Ni machungu, Bado wimbo wangu: Karibu na Mungu Karibu na Ewe, Mungu wangu! 2. Ningali njiani Kumekuchwa, Jiwe ndilo mto, Nasinzia. Naota usiku: Karibu na Mungu Karibu na Ewe, Mungu wangu! 3. Ngazi za mbinguni Wazishusha; Unanipa yote Kwa neema; Waniita juu Karibu na Mungu Karibu na Ewe, Mungu wangu! 4. Kukicha nasifu, Wastahili; Nayosimamisha Ni Betheli, Kama kumbukumbu; Karibu na Mungu Karibu na Ewe, Mungu wangu! 5. Kisha kwa furaha Nikipaa, Nifike mbinguni Kwako tena. Bado wimbo wangu: Karibu na Mungu Karibu na Ewe, Mungu wangu! Maandishi: Sarah F. Adams, 1805–1848 Muziki: Lowell Mason, 1792–1872 Mafundisho na Maagano 88:63 Mwanzo 28:10–22