174 O! Kisima Cha Baraka Kwa kuomba 1. O! Kisima cha baraka, Imbisha moyo wangu; Tiririko za rehema, Zaniita kusifu. [Chorus] Nifundishe tenzi nzuri, Ziimbwazo uliko; Mlima – wangu msingi — Nasifu pendo lako. 2. Naita Ebenezeri, Hapa nimefikia, Nako kwa yako mapenzi, Nyumbani nitafika. [Chorus] Kupotea ni mwepesi, Hata kumwacha Mungu; Moyo wangu, Ee Mwokozi, Ufunge kwako juu. 3. Alinitafuta Yesu Nikiwa ugenini; Akamwaga yake damu Kunitoa jangani. [Chorus] Kupotea ni mwepesi, Hata kumwacha Mungu; Moyo wangu, Ee Mwokozi, Ufunge kwako juu. 4. O! Yanilazimu kuwa Daima mwiwa wako! Ufungavyo wako wema, Nifunge wangu moyo. [Chorus] Kupotea ni mwepesi, Hata kumwacha Mungu; Moyo wangu, Ee Mwokozi, Ufunge kwako juu. Maandishi: Robert Robinson, 1735–1790 Muziki: John Wyeth, 1770–1858 1 Samweli 7:7–12 Alma 5:26–27