139
Tusonge Mbele
Kwa shauku
1. Tusonge mbele kwenye kazi ya Bwana,
Ndipo tukaipate zawadi tukifa;
Katika vita tuushike upanga,
Upanga wa ukweli.
[Chorus]
Jipe moyo shinda adui
Msihofu, Bwana yu nasi
Hatutawasikiliza waovu
Tutamtii Bwana Mungu.
2. Hatutasita ingawa tu wachache
Tunapolinganishwa na adui kule;
Katika Bwana nguvu yake tupate
Kutetea ukweli.
[Chorus]
Jipe moyo shinda adui
Msihofu, Bwana yu nasi
Hatutawasikiliza waovu
Tutamtii Bwana Mungu.
3. Hatutahofu tunapotenda mema,
Kwa sababu Bwana yu karibu daima;
Katika shida yeye atuwezesha
Tuushike ukweli.
[Chorus]
Jipe moyo shinda adui
Msihofu, Bwana yu nasi
Hatutawasikiliza waovu
Tutamtii Bwana Mungu.
Maandishi na muziki: Evan Stephens, 1854–1930