189
Nahisi Upendo
Kwa hisia
1. Nahisi upendo
Wa Bwana u karibu.
Nuru yake ipo
Kwenye kila kitu.
[Chorus]
Nitamtii Bwana
Maishani mwangu.
Nahisi upendo
Anipao Mwokozi.
2. Nahisi upendo
Unanikumbatia,
Na ninaposali,
Najawa furaha.
[Chorus]
Nitamtii Bwana
Maishani mwangu.
Nahisi upendo
Anipao Mwokozi.
3. Nahisi upendo
Anaponibariki.
Moyo ninampa
Wangu Mchungaji.
[Chorus]
Nitamtii Bwana
Maishani mwangu.
Nahisi upendo
Anipao Mwokozi.
4. Upendo wa Bwana
Nitasambaza kote.
Nitahudumia,
Baraka nipate.
[Chorus]
Nitamtii Bwana
Maishani mwangu.
Nahisi upendo
Anipao Mwokozi.
Maandishi: Ralph Rodgers Mdogo, 1936–1996; K. Newell Dayley, kuz. 1939; na Laurie Huffman, kuz. 1948
Muziki: K. Newell Dayley, kuz. 1939
© 1978, 1979 na K. Newell Dayley. Inatumika kwa ruhusa. Haki zote zimehifadhiwa. Wimbo huu ni kwa matumizi ya kawaida, ya kanisa yasiyo ya kibiashara au matumizi ya nyumbani.
Yohana 15:10–12