136
Ee Mungu, Angaza
Kwa uchangamfu
1. Ee Mungu, angaza
Kwa uwezo wako,
Kusudi wezesha
Lisambazwe neno;
Ufunuo utujie,
Watu ukweli wajue.
2. Yalete karibu
Mataifa yote;
Acha kila mtu
Kanuni ashike.
Mungu Baba, simamia
Kwa takatifu sheria.
3. Utukufu wako,
Wote wauone,
Dunia iwepo
Na waongofuwe.
Libariki na Kanisa,
Jaza dunia na wema.
4. Kwa Mungu pekee,
Ndiye Mtukufu,
Haleluya kwake
Aishiye juu;
Sifuni wote mlipo,
Baba, Mwana, naye Roho.
Maandishi: William Hurn, 1754–1829
Muziki: John Darwall, 1731–1789
Isaya 60:1–3