57
Nifuate
Kwa unyenyekevu
1. “Nifuate,” alisema.
Nyayo zake kufuata,
Tuwe pamoja naye tu
Mwana Mpendwa wa Mungu.
2. “Nifuate,” semi fupi,
Bali mwanga wa ukweli
Upo kwenye hili neno
Ili kuwatia moyo.
3. Je, yatosha tu kujua
Twapaswa kumfuata,
Kwenye bonde la machozi?
La hasha, hata mbinguni.
4. Siyo tu kumfuata
Tukiwa kwenye dunia,
Hata tukiwekwa huru
Na Bwana turithi mbingu.
5. Ni lazima kuisaka
Njia ya kuendelea
Kumtafuta Mwokozi
Katika yoyote hali.
6. Enzi, himaya na nguvu,
Na utukufu ni vyetu,
Tukilitii milele,
Neno lake, “Nifuate.”
Maandishi: John Nicholson, 1839–1909
Muziki: Samuel McBurney, 1847–1909
Mathayo 4:19