78
Kwa Upole Twaimba
Kwa unyenyekevu
1. Kwa upole twaimba,
Sabato yaja tena.
Tupumzike,
Tupumzike,
Na tushukuru Mungu
Baraka atupaye,
Baraka atupaye.
2. Ndiyo siku teule,
Mungu tumtafute,
Ni thawabu,
Ni thawabu,
Na tule sakramenti
Kumkumbuka Yesu,
Kumkumbuka Yesu.
3. Tuongeze sauti
Tuletapo zawadi
Ya upole,
Ya upole,
Kama dhabihu yetu
Ni kwa neema yake,
Ni kwa neema yake.
4. Ni mtukufu Kristo;
Ni zuri lake neno:
Fanya toba,
Fanya toba;
Japo dhambi nyekundu,
Msamaha atoa.
Msamaha atoa.
Maandishi: William W. Phelps, 1792–1872. Yalijumuishwa katika kitabu cha kwanza cha nyimbo za Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho, 1835.
Muziki: Thomas C. Griggs, 1845–1903