110
Mwokozi Uvaaye Taji la Miiba
Kwa kutafakari
1. Mwokozi uvaaye
Taji la miiba,
Mateso ubebaye,
Ya kebehi kubwa.
Wakuputa askari;
Wakunywesha nyongo;
Juu msalabani
Wateswa kwa kifo.
2. Hakuna mwenye dhambi
Aliye baniwa,
Utukufu kuhisi
Na kuokolewa.
Wa kusaliti wapo,
Wajua pendowe;
Nao wakuuao
Neema i bure.
3. Dhabihu ya ajabu
Imelipa deni;
Rehema yako ndefu
Ipo duniani.
Japo mwovu hudhuru,
Tu vitani bado,
Sasa hatuna hofu,
Twamwamini Kristo.
4. Sifa gani tutoe
Kushukuru, Bwana?
Msalabani pale
Juu ulifia,
Kwa mpango wa Mungu
Kuokoa nafsi.
Kwako mpendwa Yesu,
Twaleta hisani.
Maandishi: Karen Lynn Davidson, 1943–2019. © 1985 IRI
Muziki: Hans Leo Hassler, 1564–1612; umefanyiwa marekebisho na J. S. Bach, 1685–1750