80
Kwenye Siku ya Bwana
Kwa kutafakari
1. Kumkumbuka Mwanao,
Tunakusanyika kwako
Kwa pamoja tunasali,
Na kujifunza injili.
Na kwenye siku ya Bwana,
Uwe nasi tunaomba.
2. Muda wote tukuwaze
Pia na wapendwa wote.
Kwa yote tuyafanyayo
Tusali bila kikomo.
Na kwenye siku ya Bwana,
Nyumbani kwetu kawia.
3. Tupate muda mzuri
Wa nguvu yako kuhisi,
Tutii sauti ndogo,
Tufanye mapenzi yako.
Na kwenye siku ya Bwana,
Nyoyoni mwetu bakia.
Maandishi: Paul L. Anderson, kuz. 1946
Muziki: Lynn R. Carson, kuz. 1942 © 1983 na Lynn R. Carson na Paul L. Anderson. Wimbo huu wa dini ni kwa matumizi ya kawaida, ya kanisa yasiyo ya kibiashara au matumizi ya nyumbani.