37
Tuongoze Ee Yehova
Kwa sifa
1. Tuongoze Ee Yehova,
Tufikishe Sayuni.
Tu dhaifu, U muweza;
Una nguvu zaidi.
Ewe Roho utulishe
Hadi Kristo ajapo,
Hadi Kristo ajapo.
2. Yesu fungua Sayuni;
Baraka tele zije.
Nguzo ya moto na wingu
Njiani zitulinde.
Mkombozi, Mkombozi,
Ilete siku njema!
Ilete siku njema!
3. Ardhi itikisikapo,
Woga wetu tuliza;
Maangamizo yajapo,
Tubakie salama,
Tukisifu, tukiimba,
Utukufu ni kwako,
Utukufu ni kwako.
Maandishi: William Williams, 1717–1791. Ubeti wa kwanza yametafsiriwa na Peter Williams, 1722–1796. Yalijumuishwa katika kitabu cha kwanza cha nyimbo za Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho, 1835.
Muziki: John Hughes, 1873–1932
Kutoka 13:21–22