Muziki
Nyenyekea


63

Nyenyekea

Kwa utulivu

1. Nyenyekea ushindwapo, Bwana atakuongoza,

Atakuongoza na kuyajibu maombi.

Nyenyekea uombapo, Bwana atakubariki,

Atakubariki kwani hakika hujali.

2. Nyenyekea kwenye wito, Bwana atakufundisha,

Kutumikia watu, kwa pendo la upole.

Nyenyekea tamanio, Bwana atakufikisha,

Atakufikisha uishi naye milele.

Maandishi na muziki: Grietje Terburg Rowley, 1927–2015. © 1985 IRI

Mafundisho na Maagano 112:10

Etheri 12:27

Chapisha