183
Akamtuma Mwanaye
Kwa hisia
Baba angetufunzaje kuhusu upendo?
Akamtuma Mwanaye kutupa mfano.
Baba angetufunzaje njia ya kupita?
Akamtuma Mwanaye kuonyesha njia.
Baba angetufunzaje kuhusu mauti?
Akamtuma Mwanaye ashinde kaburi.
Baba anatutakaje? Imeandikwaje?
Kwa imani, kama Yesu, tupende wengine.
Tuishije? Kama Yesu.
Maandishi: Mabel Jones Gabbott, 1910–2004
Muziki: Michael Finlinson Moody, kuz. 1941
© 1982 na Mabel Jones Gabbott na Michael Finlinson Moody. Mpangilio © 1989 IRI. Wimbo huu ni kwa matumizi ya kawaida, ya kanisa yasiyo ya kibiashara au matumizi ya nyumbani.
Yohana 3:16
Yohana 13:15