53
Bwana, Dhoruba Yavuma
Kwa hamasa
1. Bwana, dhoruba yavuma!
Mawimbi ni makali!
Na giza limetanda mbingu.
Hifadhi ipo mbali.
Hujali twaangamia?
Walalaje foo,
Hali kila dakika yatisha
Na tishio la kifo?
[Chorus]
Upepo, mawimbi yaitika:
Nyamaza.
Ghadhabu ya tufani, iwe
Pepo chafu, watu au chochote,
Hakuna maji ya kumdhuru
Bwana wa bahari, nchi, mbingu.
Vyote vitakuitikia:
Nyamaza, tulia.
Vyote vitakuitikia:
Tulizana.
2. Bwana, kwa majonzi mengi
Leo nanyenyekea.
Moyo umejaa taabu.
Niokoe, naomba!
Mabubujiko ya dhambi
Yalemea roho,
Nafa maji! Nazama! Ee Bwana.
Ninyoshee mkono!
[Chorus]
Upepo, mawimbi yaitika:
Nyamaza.
Ghadhabu ya tufani, iwe
Pepo chafu, watu au chochote,
Hakuna maji ya kumdhuru
Bwana wa bahari, nchi, mbingu.
Vyote vitakuitikia:
Nyamaza, tulia.
Vyote vitakuitikia:
Tulizana.
3. Bwana, vitisho vyakoma.
Hali sasa tulivu.
Jua la akisi ziwani,
Moyoni sina hofu.
Kawia, Bwana mpendwa!
Nitoe upweke,
Nifikie bandari ya kheri
Pwani nipumzike.
[Chorus]
Upepo, mawimbi yaitika:
Nyamaza.
Ghadhabu ya tufani, iwe
Pepo chafu, watu au chochote,
Hakuna maji ya kumdhuru
Bwana wa bahari, nchi, mbingu.
Vyote vitakuitikia:
Nyamaza, tulia.
Vyote vitakuitikia:
Tulizana.
Maandishi: Mary Ann Baker, 1831–1921
Muziki: H. R. Palmer, 1834–1907