Muziki
Yesu Angekuwa Hapa


191

Yesu Angekuwa Hapa

Kwa kutafakari

1. Yesu angekuwa hapa,

Ningeyafanya haya?

Ningemkumbuka zaidi na kutenda mema?

Ningeiga mifanoye?

Ningeishi vizuri kama ningemuona Mwokozi,

Karibu nami?

2. Yesu angekuwa hapa,

Ningeyasema haya?

Ningechunga maneno kama angekuwa hapa?

Ningetangaza injili?

Ningesema mazuri kama ningemuona Mwokozi,

Karibu nami?

3. Yu karibu nami,

Roho ashuhudia

Na kwavile anipenda hivyo ananilinda,

Ndiyo, nitakuwa mtu achaguaye haki

kama ningemuona

Mwokozi karibu nami.

Maandishi na muziki: Sally DeFord, kuz. 1959. © 2007 na Sally DeFord. Haki zote zimehifadhiwa. Wimbo huu ni kwa matumizi ya kawaida, ya kanisa yasiyo ya kibiashara au matumizi ya nyumbani. Notisi hii lazima ionekane kwenye kila nakala iliyotolewa.

1 Yohana 4:14

Mafundisho na Maagano 43:34

Chapisha