7
Israeli, Mnaitwa
Kwa ari
1. Israeli, mnaitwa
Na Mwenyezi mtubu.
Babiloni yaanguka;
Inakuja hukumu.
Njooni humu Sayuni,
Kabla yake gadhabu.
Njooni humu Sayuni,
Kabla yake gadhabu.
2. Israeli, sikiliza
Bwana asema nawe!
Asubuhi yaangaza
Kwa Wateule wote.
Njooni humu Sayuni,
Ndani mfurahie.
Njooni humu Sayuni,
Ndani mfurahie.
3. Israeli, malaika
Toka juu washuka,
Wakiwapa Wema nguvu
Ya kurudi kwa Baba.
Njooni humu Sayuni,
Bwana wenu yu aja.
Njooni humu Sayuni,
Bwana wenu yu aja.
4. Israeli, msibaki
Katika dhambi zenu!
Ona! Hukumu ya haki
Yaja hivi karibu.
Njooni humu Sayuni!
Bwana Mungu msifu.
Njooni humu Sayuni!
Bwana Mungu msifu.
Maandishi: Richard Smyth, 1838–1914
Muziki: Charles C. Converse, 1832–1918