69
Ushuhuda
Kwa kutafakari
1. Ushuhuda wake Roho,
Kwa wanaojua,
Umeniinua kwako,
Ewe Mungu Baba.
2. Najua upo mbinguni.
Atawala Yesu.
Najua yupo nabii
Kwa faida yetu.
3. Moyo wangu umejaa
Roho asemaye.
Bwana, niwe mpya kwako
Na kwangu ukae.
4. Nipatapo ushuhuda,
Hupoza machungu.
Mwonekano wa mbinguni,
Huwa wazi kwangu.
Maandishi: Loren C. Dunn, 1930–2001. © 1985 IRI
Muziki: Michael Finlinson Moody, kuz. 1941. © 1985 IRI