162
Mahekalu ya Sayuni
Kwa ujasiri
1. Mahekalu ya Sayuni
Yang’ara utukufu,
Njia ya kwenda mbinguni,
Alama ya uungu.
Taswira ya kuvutia
Yatuita kuomba;
Watiifu wa ahadi,
Pale tutatumika.
2. Mungu Baba wa rehema,
Tutakase twaomba;
Bariki dhamira yetu
Ya ndugu kuokoa,
Hadi siku watiifu,
Wote tuliofungwa
Kwa pingu za selestia,
Tuziimbe hosana.
3. Mbingu, imba kwa sauti,
Nyimbo za kumsifu
Mfalme Imanueli!
Imba Watakatifu!
Milima ishangilie
Na konde zifurahi,
Nyota nazo zimsifu
Ameshinda kaburi.
Maandishi: Archibald F. Bennett, 1896–1965. © 1948 IRI
Muziki: Alexander Schreiner, 1901–1987. © 1948 IRI