70 Tubarikie Mfungo Kwa hamasa 1. Bwana tunakusujudu, Mbele zako twaja, Tunaomba kwa sauti— Je, utaongea? [Chorus] Tubarikie mfungo Na nafsi ulishe, Ili ukawe na sisi Tufurahi nawe. 2. Tumelisha wahitaji, Maskini twawapa, Tukawalaki wageni— Je, utaongeza? [Chorus] Tubarikie mfungo Na nafsi ulishe, Ili ukawe na sisi Tufurahi nawe. 3. Kama mashahidi twaja Kukupa shukrani, Kwa kutenda miujiza, Bwana tubariki. [Chorus] Tubarikie mfungo Na nafsi ulishe, Ili ukawe na sisi Tufurahi nawe. Maandishi: John Sears Tanner, kuz. 1950. © 1985 IRI Muziki: James B. Welch, kuz. 1950. © 1985 IRI Isaya 58:6–11 Mafundisho na Maagano 59:12–21