142
Tumeitwa Kumtumikia
Kwa ujasiri
1. Tumeitwa kumtumikia
Mwenyezi tumshuhudie,
Tuhubiri injili ya Bwana,
Upendo tutangaze.
[Chorus]
Mbele, kila mara, tumtukuze Bwana;
Mbele, kila mara, tumtukuze Bwana;
Mbele, twende mbele, ushindi tukiimba.
Mungu ni nguvu, twendeni mbele
Kutumikia.
2. Tumeitwa tujue baraka
Sisi watoto wa Mfalme
Na tunamwabudu kwa furaha,
Twakiri jina lake.
[Chorus]
Mbele, kila mara, tumtukuze Bwana;
Mbele, kila mara, tumtukuze Bwana;
Mbele, twende mbele, ushindi tukiimba.
Mungu ni nguvu, twendeni mbele
Kutumikia.
Maandishi: Grace Gordon, yamebadilishwa
Muziki: Adam Geibel, 1855–1933