64
Nipe Uongofu
Kwa sala
1. Nipe uongofu,
Nijutie dhambi,
Nipe stahamala,
Nijitahidi,
Nipe uelewa
Nidhamirie.
Nipe ukarimu
Nihudumie.
2. Nipe shukurani
Nisimsahau,
Nipe moyo safi
Nimuabudu,
Nipe sikitiko,
Nilie Naye,
Nipe usikivu,
Nimtukuze.
3. Nipe utakaso,
Mbinguni nifike,
Nipe na usafi,
Dhambi nishinde.
Nipe ustahili,
Mwenye kufaa.
Nipe utukufu—
Ulivyo Bwana.
Maandishi na Muziki: Philip Paul Bliss, 1838–1876