178
Nalipenda Hekalu
Kwa kutafakari
1. Nalipenda hekalu.
Nitaenda huko
Kuabudu, kuomba,
Kumhisi Roho.
Hekalu ni nyumba ya Mungu,
Nyumba ya utukufu.
Najiandaa ujanani,
Ndio wajibu wangu.
2. Nalipenda hekalu.
Nitaenda ndani.
Niagane na Baba,
Niwe wa kutii.
Kwani hekalu ni mahali
Tunapounganishwa.
Familia ni za milele,
Hivyo nashuhudia.
Maandishi na Muziki: Janice Kapp Perry, kuz. 1938
© 1980 na Janice Kapp Perry. Wimbo huu ni kwa matumizi ya kawaida, ya kanisa yasiyo ya kibiashara au matumizi ya nyumbani.