1. Kama Nefi, tumezaliwa
Kwa wazazi wamchao Bwana.
Tumefunzwa, tunabidii
Katika kuzitii amri.
[Chorus]
Tu kama jeshi la Helemani.
Tumefunzwa zamani.
Tu wamisionari wa Bwana
Kutangaza ukweli.
2. Kwa ajili ya siku hizi
Tumeitwa kuilinda haki.
Tunakubali wito wake:
“Nendeni mkatumikie.”
[Chorus]
Tu kama jeshi la Helemani.
Tumefunzwa zamani.
Tu wamisionari wa Bwana
Kutangaza ukweli.
3. Tunajua wake mpango
Kupitia sala naye Roho.
Siku zote tuwe tayari
Kote kusambaza injili.
[Chorus]
Tu kama jeshi la Helemani.
Tumefunzwa zamani.
Tu wamisionari wa Bwana
Kutangaza ukweli.
Maandishi na muziki: Janice Kapp Perry, kuz. 1938
© 1983 na Janice Kapp Perry. Wimbo huu ni kwa matumizi ya kawaida, ya kanisa yasiyo ya kibiashara au matumizi ya nyumbani.