43
Twamjia Bwana Kuomba Baraka
Kwa furaha
1. Twamjia Bwana kuomba baraka;
Hukanya, hutupa mapenzi yake;
Sasa wasumbufu wakoma maovu.
Bwana tumsifu;
Yu na waja wake.
2. Yu nasi kutuongoza, Mungu wetu,
Falme kuitunza na kustawisha;
Siku hadi siku vita tumemudu;
Bwana, upo nasi;
Tukuzwa daima!
3. Tunakusifu, kiongozi mshindi,
Na tunaomba utuhami tena.
Tuepushe sote na adui yule.
Usifiwe juu!
Tuhurishe Bwana!
Maandishi: Hajulikani, Uholanzi, mnamo 1626; yametafsiriwa na Theodore Baker, 1851–1934
Muziki: Hajulikani, Uholanzi, mnamo 1625; umepangiliwa na Edward Kremser, 1838–1914
Zaburi 100:4–5
Isaya 12:1–6