86 Bwana, Kwa Baraka Zako Kwa kutafakari 1. Bwana, kwa baraka zako, Twaenda na amani; Tupe neema, upendo Ndipo tuwe washindi. Tupe nguvu, tupe nguvu Ya kupita nyikani. Tupe nguvu, tupe nguvu Ya kupita nyikani. 2. Tunakushukuru, Bwana Kwa kutupa injili. Ukombozi ukaleta Mioyo ifurahi. Kwa ukweli, kila mara Tuwe nayo imani. Kwa ukweli, kila mara Tuwe nayo imani. Maandishi: John Fawcett, 1740–1817 Muziki: Jean-Jacques Rousseau, 1712–1778 Zaburi 31:23–24 Mafundisho na Maagano 6:13