Muziki
Ni Mwanangu Mpendwa


184

Ni Mwanangu Mpendwa

Kwa hisia

1. Kwenye maji ya Yordani

Yesu alibatizwa,

Mungu Baba akasema:

[Chorus]

“Ni Mwanangu Mpendwa. Mfuate!”

2. Wanefi walivyomwona

Mwokozi anashuka,

Baba alishuhudia:

[Chorus]

“Ni Mwanangu Mpendwa. Mfuate!”

3. Ndipo Joseph akamwona

Mungu Baba na Mwana,

Yesu akatambulishwa:

[Chorus]

“Ni Mwanangu Mpendwa. Mfuate!”

4. Nikisoma maandiko,

Maneno yake Bwana,

Nitamsikia Mungu:

[Chorus]

“Ni Mwanangu Mpendwa. Mfuate!”

Maandishi: Marvin K. Gardner, kuz. 1952

Muziki: Vanja Y. Watkins, kuz. 1938

© 1987 Vanja Y. Watkins na Marvin K. Gardner. Intatumika kwa ruhusa. Mafundisho na Maagano 18:34–36 Wimbo huu ni kwa matumizi ya kawaida, ya kanisa yasiyo ya kibiashara au matumizi ya nyumbani.

Mathayo 3:16–17

3 Nefi 11:6–8

Joseph Smith—Historia ya 1:17

Mafundisho na Maagano 18:34–36

Chapisha