14 Nabii Mpendwa Kwa hamasa 1. Nabii mpendwa, twamuomba Akupe faraja, Mungu Baba. Miaka ijavyo na uzee, Na mwangaza wako uangaze, Na mwangaza wako uangaze. 2. Tunakuombea mioyoni, Ukapewe nguvu na Mwokozi Ya kutuongoza kila siku, Ya kuiangaza njia yetu, Ya kuiangaza njia yetu. 3. Tunakuombea, twakupenda, Na maombi yetu yasikika. Ubarikiwe na Mungu wetu, Na akupatie kila kitu, Na akupatie kila kitu. Maandishi: Evan Stephens, 1854–1930 Muziki: H. A. Tuckett, 1852–1918; umefanyiwa marekebisho na Evan Stephens, 1854–1930 Mafundisho na Maagano 107:22