172
Watoto wa Mungu
Wanaume
Kwa ufahari
1. Watoto wa Mungu na wenye ukuhani,
Mueneze neno na mkusanye watu.
Sasa imeanza kazi,
Wakusanye Israeli,
Na warudi Sayuni kumsifu.
2. Njooni kondoo, msikilize Bwana,
Mvune baraka zilizotabiriwa
Na manabii wa kale,
Kwamba mtaishi naye
Awalete Sayuni mumsifu.
3. Tubu, mbatizwe na mtasamehewa,
Mumpate Roho, muwe kitu kimoja.
Muombeni msamaha;
Naye atajibu sala
Na mrudi Sayuni kumsifu.
4. Yatakapokwisha majonzi na mateso,
Roho zitaenda kungoja Ufufuo;
Na mtakaa pamoja,
Mbinguni kwenye furaha,
Mtakaa Sayuni kumsifu.
Maandishi: Thomas Davenport, 1815–1888
Muziki: Orson Pratt Huish, 1851–1932