20
Njooni Enyi Watakatifu
Kwa ujasiri
1. Njooni enyi Watakatifu;
Kwa moyo tembea.
Safari yaweza kuwa ngumu,
Neema yatosha.
Ni bora tuvumilie
Wasiwasi tuondoe;
Fanya hivi, mfurahi—
Ni shwari! Ni shwari!
2. Je, tulijutie fungu letu?
Si hivyo; ni sawa.
Je, tuitegemee thawabu,
Vitani twatega?
Dhamiria; jipe moyo.
Mungu wetu nasi yupo;
Punde itanenwa hivi—
Ni shwari! Ni shwari!
3. Tutayapata makao mapya,
Sayuni tufike,
Ambapo hatutasumbuliwa;
Baraka tupate.
Tutapaza nyimbo zetu
Kumsifu Mungu wetu;
Na tutasema zaidi—
Ni shwari! Ni shwari!
4. Na tukifa kabla ya kufika,
Hakika! Ni shwari!
Tutakuwa huru, bila shida,
Tuishi peponi!
Na kama tutakuwepo
Kuliona kimbilio
Tutaimba jinsi gani—
Ni shwari! Ni shwari!
Maandishi: William Clayton, 1814–1879
Muziki: Wimbo wenye asili ya Uingereza