131 Ifanye Njia Ng’avu Kwa uchangamfu 1. Ifanye njia ng’avu, Jaza nafsi na nuru, Je, moyo u tayari? Gizani pawe mwanga, Vivuli kutoweka, Kama moyoni unanuru. [Chorus] Je, moyo u tayari? Toa mwali mng’avu Usiku uwe siku; Utavuna amani, Kama moyoni unanuru. 2. Nena neno tulivu Kwenye moyo wa hofu, Je, moyo u tayari? Wala si jambo dogo, Neema iletwayo, Kama moyoni unanuru. [Chorus] Je, moyo u tayari? Toa mwali mng’avu Usiku uwe siku; Utavuna amani, Kama moyoni unanuru. 3. Lifanye jambo jema Kwa yule mwenye haja, Je, moyo u tayari? Mzigo mtwalie, Shida mpunguzie Kama moyoni unanuru. [Chorus] Je, moyo u tayari? Toa mwali mng’avu Usiku uwe siku; Utavuna amani, Kama moyoni unanuru. 4. Kuishi kwa furaha Duniani pa shida, Je, moyo u tayari? Utang’ara upendo, Mtukufu mng’ao, Kama moyoni unanuru. [Chorus] Je, moyo u tayari? Toa mwali mng’avu Usiku uwe siku; Utavuna amani, Kama moyoni unanuru. Maandishi: Helen Silcott Dungan, 1855–1914 Muziki: James M. Dungan, 1851–1925 Mosia 2:17, 41 1 Petro 3:8–12