133 Tenda Mema Kwa uthabiti 1. Tenda mema; imeanza siku, Mwanga na uhuru vyaingia. Na malaika waandika juu Kila tendo, hivyo tenda mema. [Chorus] Tenda mema; matokeo badaye. Kwa nguvu uhuru pigania; Kwa moyo shupavu uendelee. Mungu yupo, hivyo tenda mema! 2. Tenda mema; zafunguka pingu. Wafungwa uhuru wamepata. Kwa imani hawana maumivu. Ukweli wasonga; tenda mema. [Chorus] Tenda mema; matokeo badaye. Kwa nguvu uhuru pigania; Kwa moyo shupavu uendelee. Mungu yupo, hivyo tenda mema! 3. Tenda mema; uoga uache. Songa mbele, lengo waliona. Nayo machozi yatakwisha punde. Kuna baraka kutenda mema. [Chorus] Tenda mema; matokeo badaye. Kwa nguvu uhuru pigania; Kwa moyo shupavu uendelee. Mungu yupo, hivyo tenda mema! Maandishi: Hajulikani, The Psalms of Life, Boston, 1857 Muziki: George Kaillmark, 1781–1835 Kumbukumbu la Torati 6:17–18 Helamani 10:4–5