62
Iwapi Amani?
Kwa kutafakari
1. Iwapi amani?
Si mtulivu.
Mwingine hawezi kuniponya.
Nichomwapo moyo, niwapo mwovu,
Najitenga kando
Kuchunguza?
2. Niwapo na dhiki,
Pindi mchovu,
Ninapohitaji kimbilio,
Yupo wa kuponya yale machungu.
Nani muelewa?
Yeye Kristo.
3. Anijibu yeye,
Kilio changu,
Niwe Gethsemane, ni Rafiki.
Amani huupa usihi wangu.
Ni mwema daima,
Haishiwi.
Maandishi: Emma Lou Thayne, 1924–2014. © 1973 IRI
Muziki: Joleen G. Meredith, kuz. 1935. © 1973 IRI