132
Tuambizane Mema Daima
Kwa dhati
1. Tuambizane mema daima
Nyumbani au popote;
Kama ndege kati ya maua
Sauti zipokelewe.
Yafariji kwenye majonzi,
Yatutia moyo nguvu,
Na penye wingu la huzuni,
Huleta pendo ng’aavu.
[Chorus]
Kila neno jema litatukumbusha,
Labakia kama kito.
Tuambizane mema daima;
Yawa taswira ya moyo.
2. Kama mwale wa jua Sayuni
Nafsi yanafurahisha;
Kama kisima cha maji safi,
Taratibu yatuwama.
Hivyo kwa sauti karimu,
Urafiki tuujenge,
Mioyo iwe mikunjufu
Na kufurahi popote.
[Chorus]
Kila neno jema litatukumbusha,
Labakia kama kito.
Tuambizane mema daima;
Yawa taswira ya moyo.
Maandishi: Joseph L. Townsend, 1849–1942
Muziki: Ebenezer Beesley, 1840–1906
Waefeso 4:29–32
Mithali 16:24