16
Msikilize Nabii
Kwa furaha
1. Msikilize nabii
Na neno la Mungu,
Ufurahie ukweli
Uimbe kwa nguvu.
Tumeshaipata njia
Ya wale wa mwanzo.
Nabii mpya katumwa
Kurejesha neno.
2. Giza nene lilitanda
Kote duniani,
Bwana amelifukuza,
Mungu anaishi.
Kupitia njama mbovu
Zikawapotosha,
Lakini Watakatifu
Wamepata njia.
3. Hawategemei mtu
Na yake mikono.
Wamkataao Yesu,
Laana ni yao.
Anasema Mkombozi,
“Nifuate, njoo,
Neno langu ulitii
Hata mpaka mwisho”.
4. Sikia neno la kweli
Safi vyanzo vyake.
Amri zake uzitii
Hadi uteule,
Na uvalishwe na Mungu
Taji la milele,
Utapata utukufu,
Urithi wa shangwe.
Maandishi: Joseph S. Murdock, 1822–1899. Ubeti wa nne, Bruce R. McConkie, 1915–1985. © 1985 IRI
Muziki: Joseph J. Daynes, 1851–1920