119
Mji Mwema, Bethlehemu
Kwa utulivu
1. Mji mwema, Bethlehemu,
Tuli watulia.
Ulalapo, nyota nazo
Zinapita kimya;
Na gizani yang’aa
Nuru ya milele.
Tumaini za vizazi
Zatimia nawe.
2. Hivyo Kristo azaliwa;
Malaika juu
Wakalinda kwa upendo
Wakistaajabu.
Nyota za alfajiri
Ujio tangaza,
Imbeni sifa kwa Mungu,
Kwa watu faraja.
3. Kimyakimya, hivyo ndivyo
Zawadi hupewa!
Mungu atoa kwa watu
Za kwake baraka.
Hawataona aja;
Ila duniani,
Kote wapole walipo
Kristo aja kweli.
Maandishi: Phillips Brooks, 1835–1893
Muziki: Lewis H. Redner, 1831–1908