36
Msingi Imara
Kwa heshima
1. Msingi imara, Watakatifu,
Wajengwa kwa neno la Bwana kwenu!
Aseme nini zaidi ya haya—
Nani kwa Mwokozi, nani kwa Mwokozi,
Nani kwa Mwokozi kakimbilia?
2. Kwa hali zozote— ugonjwa, afya,
Umaskini na wingi wa neema,
Barani, majini, nyumbani na ng’ambo—
Zidaivyo siku, zidaivyo siku,
Zidaivyo siku, kudra huavyo.
3. Msiogope kwani niko nanyi,
Ni Mungu wenu, nawapa auni.
Nitawaimarisha, msimame—
Kwa mkono wangu, kwa mkono wangu,
Kwa mkono wangu— milele yote.
4. Nikuitapo, vilindi kupita
Majonzi kwako hayatafurika,
Kwani niko nawe, kukubariki,
Na kuzitakasa, na kuzitakasa,
Na kuzitakasa, zako huzuni.
5. Majaribu ya moto upatapo,
Neema yangu, itoshayo, ipo.
Moto hutadhuru; nakusudia
Kuzichoma taka, kuzichoma taka,
Kuzichoma taka, kukusafisha.
6. Hadi uzeeni huthibitisha
Upendo wangu ulioimara;
Kisha, mvi zirembapo utosi,
Ni mwanakondoo, ni mwanakondoo,
Ni mwanakondoo mwangu moyoni.
7. Nafsi iliyotegemea Bwana
Kamwe kwa adui sitoitupa;
Hata jehanamu iitikise,
Kamwe sithubutu, kamwe sithubutu,
Kamwe sithubutu itelekezwe!
Maandishi: Yanahusishwa na Robert Keen, mnamo 1787. Yalijumuishwa katika kitabu cha kwanza cha nyimbo za Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho, 1835.
Muziki: Unahusishwa na J. Ellis, mnamo 1889