19
Msafiri Kwa Miguu
Kwa utulivu
1. Msafiri kwa miguu
Safarini twakutana,
Huomba nimnusuru
Sijaweza kumnyima.
Hamu kujua si nayo,
Atokako, aendako;
Lakini machoni mwake
Huniteka na mboniye.
2. Nilipokuwa nakula,
Akaja; pasipo hali,
Akiwa na njaa sana,
Nikampa; kabariki,
Akala na akanipa
Tena, sikutegemea.
Nilipokula kwa hamu,
Kikawa kitamu kwangu.
3. Nikamuona mtoni;
Hakuwa na nguvu kunywa.
Yakitiririka maji,
Kikombe nikakichovya.
Nikamvuta karibu;
Akanywa, tena kwa hamu.
Mara ya tatu, kanipa;
Nikanywa, kiu kukata.
4. Usiku baridi kali
Na upepo ukavuma.
Nilisikia kwa mbali
Sauti ilipoita.
Nikajibu njoo kwangu.
Nikampa mto wangu,
Nikalala sakafuni,
Nikahisi ni Edeni.
5. Kapigwa na kunyang’anywa,
Katelekezwa njiani.
Pumzi nikamhuisha,
Na nikampa nusuri.
Kwa huduma akapona.
Shida zangu nikaficha
Na hata kuzisahau;
Amani ikanitibu.
6. Gerezani nikamwona,
Kashtakiwa uhaini.
Waongo niliwazima,
Kwa hizo zao kejeli.
Moyo wangu kujaribu,
Akadai pumzi yangu.
Mwili wabishia wito,
Roho yaitika, “Ndiyo!”
7. Mara tu mwangu usoni
Afichuka yule mtu.
Alama zake si ngeni;
Mwokozi yu mbele yangu.
Ndipo akaniambia,
“Nami haukuchukizwa.
Huu ni wako urithi;
Ulinitendea mimi.”
Maandishi: James Montgomery, 1771–1854
Muziki: George Coles, 1792–1858, umebadilishwa.
Wimbo uliimbwa kabla ya kifo cha kishahidi cha Nabii Joseph Smith. Tazama Historia ya Kanisa, 6:614–15.